12 Novemba 2019 - 11:35
Rais Rouhani: Uwezo wa kinyuklia wa Iran upo katika hali bora kabisa

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ustawi na maendeleo ya taifa hili katika uga wa teknolojia ya nyukllia na kusema kuwa, hii leo Iran ipo katika hali na mazingira bora kabisa kuliko wakati wowote ule katika uga wa uwezo wa teknolojia ya nyuklia.

(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa na iliyojaa hamasa ya wananchi wa mji wa Rafsanjan katika mkoa wa Kerman wa kusini mwa Iran na kuongeza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni hatua za utafiti, uhakiki na ustawi katika uga wa teknolojia ya nishati ya nyuklia umeendelea nchini Iran na hii leo kuna aina kwa aina ya mashinapewa amilifu hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, hakuna kizingiti kinachoweza kulizuia taifa hili kuendeleza uhakiki na ustawi katika uga wa teknolojia ya nishati ya nyuklia.

Aidha Rais Rouhani amesema bayana kwamba, Iran imesimama kidete na kwa uwezo wake wote mbele ya maadui na kamwe haitasalimu amri mbele yya hatua zao za kibabe na utumiaji mabavu.

Rais wa Iran amesema pia kuwa, endapo makubaliano ya nyuklia yatabakishwa na kudumu, taifa hil hapo mwakani litakuwa limefikia matunda makubwa ya kiusalama na kiulinzi na ikiwa kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa makubaliano ya JCPOA yakabakishwa na mwakani vikwazo vya silaha dhidi ya Iran vikaondolewa, basi Iran ya Kiislamu itakuwa na uwezo wa kununua na kuuza silaha.

.........
340